Habari kwa Wazazi
Wazazi ni sehemu muhimu kwa mafuzo wa yamtoto na mafanikio ya shuleni. Programu ya Elimu ya Uhamiaji ya Tennessee (TN MEP) inaamini sana umuhimu na jukumu la wazazi katika maisha ya watoto wao, na inakusudia kutoa usadizi muhimu wakusaidia wazazi. Hapo chini unaweza kupata rasilimali ambazo zinazoweza kutumiwa na wazazi na familia wahaniaji.
Kuhamasisha na Kubuni: Muungano wa Vitendo vya Mzazi Wahamaji (I2MPACT): Ushahidi unaonyesha kuwa ushiriki wa mzazi ni msingi mkubwa sana kwa ushiriki wa watoto shuleni, ukuaji wa masomo, na, kupata diploma ya shule ya sekondari au vyete vingine. I2MPACT ni muungano wa majimbo ulioanzishwa kusaidia mipango ya elimu ya wahamiaji wa mkoa (MEPs) na kuongeza ushiriki wa wazazi. Kazi za I2MPACT zimeundwa kwa familia kujifunza na kukua pamoja na mafanikio ya kielimu yanayoungwa mkono kupitia sehemu muhimu za I2MPACT: nyumba, shule, na jamii. Kujifunza zaidi tembelea www.i2mpact.org
Idara ya Elimu ya Tennessee ina upatikanaji mtandaoni wa rasilimali kwa wanafunzi na familia. Rasilimali hizi hutoa maelezo ya kina (tosha) juu ya mipango ya elimu, mtihani, na mahitaji ya wanafunzi wa Tennessee pamoja na huduma za kusaidia wazazi na wanafunzi kupitia mfumo wa elimu.
UPATIKANAJI wa ELL ni tathmini inayotumiwa na Idara ya Elimu ya Tennessee kuamua uelevu wa Kiingereza wa wanafunzi kusoma, kuandika, kusikiliza na kuzungumza kwa Kiingereza. Tathmini inaweza kusaidia wilaya za shule kuamua huduma za ziada na programu kwa wanafunzi ambao wanahitaji msaada ili kuboresha ujuzi wao wa mawasiliano kwa Kiingereza.
GearUp TN: Mkoa wa Tennessee umeunda rasilimali kadhaa zakusaidia mwanafunzi wako ili wafike chuoni na kukupa ufahamu juu ya mchakato wa kwenda chuo kikuu. Tunakuhimiza uangalie rasilimali zote zinazopatikana katika CollegeforTN.org , Kituo cha habari cha Chuo Kikuu cha Tennessee. Tovuti inajumuisha sehemu na zana tu kwa wazazi.
Ready4K Rudi kwa Rasilimali za Shule Ready4K ilimetoa rasilimali mbili kusaidia kulahisishia watoto kurudi shule. Rasilimali hizo zinapatikana kwa Kiingereza na Kihispania.
Kujifunza hesabu Nyumbani-Tembelea tovuti ya Colourin Colorado kwa michezo ya kufurahisha iliyohimizwa ya hesabu familia kucheza kwapamoja'. https://www.colorincolorado.org/learning-together-home-math